GAZA CITY : Watoto watatu wa Kipalestina wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Watoto watatu wa Kipalestina wauwawa

Wapalestina wenye silaha wamewauwa watoto watatu wa afisa mwandamizi wa ujasusi wa Palestina leo hii wakiwa ndani ya gari katika barabara iliokuwa imejaa mamia ya watoto wa shule shambulio ambalo yumkini likazusha mapigano makubwa kati ya makundi ya Kipalestina.

Katika shambulio hilo watu hao waliokuwa na silaha walimimina risasi kadhaa kwenye gari lilikouwa limewachukuwa watoto hao wa afisa ya ujasusi Baha Balousheh ambaye ni mfuasi wa wa kundi la Fatah la Rais Mahmoud Abbas wa Palestina.

Muongo mmoja uliopita Balousheh alikuwa msaili mkuu wakati wa msako wa kundi la wanamgamo wa Hamas ambalo hivi sasa ndio linaloongoza serikali ya Palestina.

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com