GAZA CITY : Kamanda wa Hamas auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Kamanda wa Hamas auwawa

Vikosi vya Israel vimempiga risasi na kumuuwa kamanda wa kundi la Hamas wakati vilipojipenyeza kwenye mji wa Gaza.

Kwa mujibu wa mashahidi wa Kipalestina mwanamke wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 70 pia aliuwawa katika mashambulizi hayo ya Israel.Tukio hilo limekuja masaa machache kufuatia shambulio la Israel kwenye gari katika mji huo wa Gaza ambapo wanamgambo wawili wa Hamas waliuwawa na watu wengine kadhaa kujeruhiwa.

Baada ya shambulio hilo la leo wanamgambo wa Kipalestina walifyatuwa maroketi mawili kwenye mji wa Israel wa Sderot na kumjeruhi vibaya mtu mmoja.

Israel imekuwa ikizidisha mashambulizi yake ya kijeshi ya hivi sasa katika Ukanda wa Gaza kwa jaribio la kukomesha mashambulizi ya maroketi ya Wapalestina ambapo mwanamke mmoja wa Israel ameuwawa wiki iliopita kutokana na mashambulizi hayo ya maroketi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com