GAZA: Chama cha Hamas chatoa wito mwandishi wa habari aachiwe huru. | Habari za Ulimwengu | DW | 16.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Chama cha Hamas chatoa wito mwandishi wa habari aachiwe huru.

Tawi la kijeshi la chama cha Wapalestina cha Hamas limetoa wito mwandishi wa habari raia wa Uingereza, Alan Johnson, aachiwe huru mara moja.

Mwandishi huyo wa habari alitekwa nyara mjini Gaza miezi mitatu iliyopita.

Tawi la Ezzedine al-Qasam limesema litachukua hatua mwafaka kuhakikisha mwandishi huyo wa habari ameachiwa huru.

Alan Johnson, ambaye ni mwandishi wa habari wa BBC, alitekwa nyara na kundi linalosemekana kuwa na uhusiano na chama cha Hamas.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com