GAZA: Al Aqsa yatishia kuwaua viongozi wa Hamas | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Al Aqsa yatishia kuwaua viongozi wa Hamas

Wapiganaji wa kundi la al Aqsa nchini Palestina, kitengo cha chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas, kwa mara ya kwanza wametishia kuwaua viongozi wa chama cha Hamas, pamoja na kiongozi aliye uhamishoni, Khaled Meshaal.

Kitisho hicho kinaashiria kuzidi kwa mivutano na kung´ang´ania madaraka kati ya chama cha Fatah na Hamas, kufuatia siku mbili za mapigano katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, ambapo wapaletina 12 waliuwawa na wengine zaidi ya 100 wakajeruhiwa.

Wakati huo huo, wapalestina wawili wamejeruhiwa mapema leo wakati ndege ya Israel ilipoishambulia karakana moja huko Khan Yunes kusini mwa Ukanda wa Gaza. Duru za usalama zinasema kombora moja limevurumishwa katika karakana hiyo na kuwajerhi watu hao wawili wanaishi karibu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com