Gaza. Abbas kuivunja serikali ya Palestina? | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Abbas kuivunja serikali ya Palestina?

Waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas amesema leo kuwa atakataa hatua zozote za rais Mahmoud Abbas za kuiondoa serikali yake, akionya kuwa juhudi kama hizo hazitapunguza hali ya wasi wasi ambayo imeleta hali ya kitisho cha kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Haniyeh amesema kuwa haitakuwa na maana kwa Abbas kuivunja serikali, akidokeza kuwa utawala wowote wa muda utakaoteuliwa na rais hautapata kuidhinishwa na bunge, ambalo linadhibitiwa kwa wingi mkubwa na chama cha Hamas.

Abbas ametoa ishara kuwa anaweza kuivunja serikali inayoongozwa na chama cha Hamas baada ya juhudi za kuunda baraza la mawaziri la umoja wa kitaifa kushindwa kutokana na Hamas kukataa kulegeza msimamo wao kuhusu Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com