Gaboni yatinga hatua ya robo fainali | Michezo | DW | 28.01.2012
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Gaboni yatinga hatua ya robo fainali

Hapo jana katika Mchuano wa Kombe la Mataifa Barani Afrika , Gabon na Tunisia kwa pamoja zimetinga katika hatua ya robo fainali. Gabon imepata tiketi ya kuingia katika hatua hiyo baada ya kuichapa Morocco mabao 3-2.

Tunisian teammates, including Aymen Abdennour (Top) embrace goalscorer Youssef Msakni (hidden) during the Africa Cup of Nations match between Morocco and Tunisia in Libreville, Gabon, 23 January 2012. EPA/STR EDITORIAL USE ONLY

Mchuano wa Marocco na Tunisia

Kwa ushindi huo wa mabao mawili kwa matatu wa Gabon dhidi ya Moroco ndio kusema imefungua pazia la kuingia katika mchuano wa robo fainali. Lakini pamoja na majeraha yaliyopatikana kwa Morocco iliaminika kujitahidi kwa kiasi cha kutosha katika kuleta matumaini ya kuendelea kudumu katika mchuano huo Kombe la Mataifa Barani Afrika.

Kasi ya Morocco ilipunguzwa pale ambapo mchezaji kiungo Bruno Mbangoyes alipomimina mkwaju mkali na kutatua nyavu ya klabu hiyo kutoka kaskazini mwa Afrika. Na kwa upande wao Gabon waliwasha dimu ya kuonesha dhahiri kuwa watatoka kidedea baada ya ushindi wake katika nusu ya kwanza pale ambapo mchezaji Daniel Cousin kwa ushirikiano wa Pierre Emerick walipoiinamisha vichwa wa mashabiki wa Morocco.

A Senegalese soccer fan wearing face paint in her country's colors waits for her team to play Angola in a group D match in the African Cup of Nations in Tamale, Ghana, Sunday, Jan. 27, 2008. (AP Photo/Alastair Grant)

Mshabiki wa Soka

Kwa kile kinachosemwa mfa maji haishi kutapatapa, katika mchuano huo wa jana Kocha wa Morocco kwa zaidi ya Eric Gerets afanya mabadiliko mara nne ikiwa ni jitihada tu, ili kujinasua katika mtego huo.

Kocha huyo Mbeligiji aliamua wiki hii kuanza kumchezesha mshambuliaji matata wa anaechezea Arsenal ambae hata hivyo alipata alipata alipata tatizo la tumbo na kumfanya aungane na vifaa vingine vya timu hiyo vilivyokuwa benchi kama Noureddine Amrabat, Mbark Bosoufa na Ossama Assaid ambao pia wamepata majeraha.

Hasimu wake Kocha wa Gabon, Gernot Rohr alikuwa na utaratibu mwingine kabisa unaonesma kama amejeruhiwa basi usimtumie.

Rais Ali Bongo wa Gabon alikuwa miongoni mwa maelfu ya waliohudhuria mchuano huo akiwa amesiti katika eneo la watu muhimu akisutia kuruka katika kiti chake na kushangilia ushindi wa timu yake.

Mwisho wa mchuano huo akionekana mwenye sura yenye tabasamu na bashasha huku kwa akili ya kawaida kabisa alionekana kama mtu mwenye kuona mchezo wa soka na hasa kombe la washindi barani Afrika kama mashindano mazuri kupia kiasi.

Morocco ilionekana kama imetawala mchezo kwa wakati wote lakini hatiame walifyata mkia katika kipindi cha pili pale ambapo nahodha Houssen Kharja alipoongzea shaka kwa tumu hiyo na baada dae kufungwa baada ya mpira wa kona na kufanya mabao mawili kwa mawili.

Naweza kusema gori tata lililopachikwa kimiani na Bruno Zita Mbanangoye na kuipa Gabon ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Morocco limeifanya timu hiyo kuingia katika robo fainali.

DW inapendekeza

 • Tarehe 28.01.2012
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13sG5
 • Tarehe 28.01.2012
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13sG5