Fury vs Klitschko sehemu ya pili
9 Aprili 2016Matangazo
Hayo yametangazwa na mwalimu wa bondia huyo Muingereza ambaye pia ni mjombake Peter Fury
Klitschko mwenye makaazi yake mjini Hamburg, Ujerumani, alipoteza mataji yake ya WBA, IBF na WBO dhidi ya Fury kupitia wingi wa pointi katika pigano lao la Dusseldorf mwezi Novemba mwaka jana. Kilikua kichapo cha kwanza kwa Muukraine huyo katika zaidi ya muongo mmoja. Fury aliye na umri wa miaka 27, anayetokea Manchester, kaskazini ya England, alipokonywa mkanda wa IBF kwa kukubali kupanda ulingoni na Klitschko katika mpambano wa marudiano.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/Reuters/DPA
Mhariri: Sessanga Iddi