1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Faru mweupe wa mwisho duniani afariki

20 Machi 2018

Faru huyo aliyeitwa Sudan amefariki kutokana na matatizo ya kiafya yaliyochangiwa na umri wake. Alifikisha miaka 45 na alikuwa akipewa matunzo maalum katika hifadhi ya wanyamapori ya Ol Pejeta, nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/2uccy
Faru Sudan
Picha: Reuters/T. Mukoya

DW  imezungumza na Paul Gathitu, msemaji mkuu wa Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori ya Kenya, na kwanza kutaka kujua sababu ya kifo cha Faru Sudan na kama kulikuwa na juhudi zozote za kuweza kuzalisha kizazi kijacho cha jamii hiyo ya wanyama kwa vile kuna faru wawili tu weupe wa kike ambao wangali hai.