1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Europa Ligi, mabingwa watetezi Atletico Madrid yaona mwezi

Sekione Kitojo22 Oktoba 2010

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Europa Atletico Madrid wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kushinda msimu huu.

https://p.dw.com/p/Pkb3
Diego Forlan, kushoto wa Atletico Madrid akishangiria bao.Picha: AP

Kandanda.

Katika  michuano   ya    ligi  ya  Europa  jana  Alhamis , viongozi  wa  ligi  ya  Ujerumani  Bundesliga, Borussia Dortmund  ilikubali  goli  la  dakika  ya  mwisho  la kusawazisha   dhidi  ya  Paris St Germain  na  kutoka  sare ya  bao  1-1. Klabu  ya  Stuttgart  ambayo  iko  mkiani  mwa Bundesliga   hadi  sasa  msimu  huu  ilipata  ushindi mwembamba  wa  bao 1-0  dhidi  ya  FC  Getafe  ya Hispania. Nayo  Bayer   Leverkusen   ilitoka  sare  ya  bila kufungana  na  Aris  Saloniki  kutoka  Ugiriki.  matokeo hayo  yanaiweka  Bayer  Leverkusen  katika  nafasi  ya  juu ya  kundi  B  wakati  Aris  imeendeleza  rekodi  yake  ya kutofungwa  nyumbani.

Mabingwa  watetezi  Atletico Madrid  ilishinda   kwa  mara ya  kwanza  msimu  huu  katika  kinyang'anyiro  hicho  kwa kuirarua  Rosenborg  kwa  mabao  3-0 , nae  Emmanuel Adebayor  alipachika  mabao  matatu  wakati  Manchester City  ilipofanikiwa  kuiangusha  Lech Poznan  ya  Poland kwa  mabao  3-1.

Emmanuel Adebayor / Togo
Emmanuel Adebayor, wa Manchester City alifumania nyavu mara tatu usiku huo.Picha: AP

Timu  ya  daraja  la  pili  nchini  Uswisi  Lausanne, ikiwa nyuma  kwa  mabao  3-1  dhidi  ya  Sparta Prague  katika dakika   ya  23, iliweza  kujikwamua   na  kutoka  sare  ya mabao  3-3  katika  matokeo  ya  kushangaza  usiku  huo ambao  timu  zote  nne  za  Italia  zilishindwa  kuwika.

Parlemo  ilifanya  vibaya  zaidi  ya  timu  nyingine  za  Italia wakati  ilipochapwa  mabao  3-0  nyumbani  na  CSKA Moscow, wakati  Napoli  walikabwa  koo  na  Liverpool  ya Uingereza  na  kutoka  sare  bila  kufungana.

Zenit St. Petersburg, VfB Stuttgart, Porto  na  Sporting zote  zilishinda  na  kuweka  rekodi  safi  ya   kushinda michezo  yao  yote  hadi  sasa  pamoja  na  CSKA Moscow.

Katika  mchezo  mwingine  wa  kundi  A Juventus  Turin ilitoka  sare  ya  bao  1-1  na  Salzburg.

Mwandishi : Sekione Kitojo / RTRE

I