1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yaitoza Facebook faini ya Euro milioni 110

Sekione Kitojo
18 Mei 2017

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya - EU imeutoza faini ya Euro milioni 110 mtandao wa kijamii wa Facebook, kwa kutoa taarifa za kupotosha wakati wa uchunguzi wa Umoja wa Ulaya mwaka 2014

https://p.dw.com/p/2d9xe
Symbolbild Facebook kauft WhatsApp
Picha: picture-alliance/dpa

Kamisheni hiyo imeituhumu Facebook kutoa taarifa potofu, ikikanusha uwezekano wa kuunganishwa kielektroniki kwa kurasa za mtumiaji za Whatsap na Facebook, ingawa mtandao huo ulifahamu kuwa uwezekano huo upo. Kamisheni ya Ulaya imesema kuwa faini hiyo inahusu taarifa hiyo ya kupotosha, lakini haiondoi ridhaa yake kwa Facebook kuinuua Whatsapp.

Kamishna wa Umoja wa Ulaya ahusikaye na sera ya ushindani Margrethe Vestager amesema uamuzi wa leo ni ujumbe kwa makampuni mengine kwamba yanapaswa kuheshimu kanuni za kibiashara za umoja huo, ikiwa ni pamoja na wajibu wa kutoa taarifa sahihi.

Mwandishi: Sekione Kitojo
Mhariri: Bruce Amani