1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ESSEN: Waziri wa Fedha wa Ujerumani, Peer Steinbrück atoa tahadhari kuhusiana na sekta ya fedha.

10 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTU

Waziri wa Fedha wa Ujerumani, Peer Steinbrück, amesema sekta ya kifedha duniani itaathirika kwa kiasi kikubwa iwapo hazina yoyote kuu ya fedha iliyotengwa kwa dharura itaanguka.

Waziri Peer Steinbrück alikuwa akizungumza katika mji wa Essen, magharibi mwa Ujerumani, mwanzoni mwa mkutano wa mawaziri saba wa fedha pamoja na wakuu wa benki kuu.

Mkutano huo wa siku mbili ulitarajiwa kutoa kipaumbele kwa masuala kadhaa likiwemo suala la hazina za dharura.

Serikali ya Ujerumani imekuwa ikitetea hazina hizo zidhibitiwe ipasavyo.

Waziri Steinbrück alielezea uwezekano wa kutanua kundi la mataifa saba, G7, ili lijumuishe China, India, Brazil na Afrika kusini kama wanachama kamili.