1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECUADOR: Raia wasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais wa jumapili

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2L

Raia nchini Ecuador wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais wa jana. Taarifa za mwanzo zimesema, Alvaro Noboa, tajiri anayebashiriwa na wengi kuwa kwenye nafasi nzuri kuweza kuibuka mshinda na mgombea, Rafael Correa, aliyesoma mambo ya uchumi nchini Marekani, wanaongoza mbele ya wagombea wengine 11 wa kiti cha urais. Hata hivyo hakuna atakayeweza kushinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi. Kulingana na matokeo kuhusu asili mia 35 ya kura zimeshahesabiwa, Alvaro Noboa, amepata asili mia 26.1 huku mpinzani wake, Rafael Correa, akipata asili mia 23,1. Itabidi ifanyike duru ya pili ifikapo tarehe 26 mwezi ujao.

Zaidi ya watu milioni 8 walitarajiwa kupiga kura.