1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Ebrahim Raisi aizuru Pakistan

23 Aprili 2024

Rais wa Iran Ebrahim Raisi yupo katika ziara rasmi ya siku tatu katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, wakati mataifa hayo mawili ya kiislam yakijaribu kuimarisha uhusiano baada ya vita katika maeneo yao ya mpakani

https://p.dw.com/p/4f6by
Pakistan
Rais wa Iran Ebrahim Rais akiwa ziarani nchini PakistanPicha: Uncredited/Prime Minister Office/AP/dpa/picture alliance

Rais wa Iran Ebrahim Raisi yupo katika ziara rasmi ya siku tatu katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, wakati mataifa hayo mawili ya kiislam yakijaribu kuimarisha uhusiano. Hatua hiyo inafuatia mashambulizi ya kijeshi ya mapema mwaka huu baina ya nchi hizo mbili katika eneo la mpakani la Balochastan.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesema Rais wa Iran Ebrahim Rais ambaye ameongozana na mkewe, jopo maalum la ujumbe linalowajumuisha mawaziri pamoja na wajumbe wengine wapo nchini humo kwa majadiliano ya kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo. 

Irans Präsident zu Staatsbesuch in Pakistan
Rais wa Iran Ebrahim Rais akiwa na mwenyeji wake Shehbaz Sharif nchini PakistanPicha: Prime Minister Office/AP/picture alliance

Soma zaidi. Iran na Pakistan zakubaliana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara 
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif imesema viongozi wote wawili walikuwa na majadiliano muhimu ya juu ya kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili huku wakikubaliana juu ya umuhimu wa juhudi za pamoja za kupamabana na ugaidi.
Pakistan na Iran zimekuwa kwenye mvutano baina yao kwa muda mrefu ingawa mvutano wa mapema mwaka huu ndio ulikuwa mkubwa zaidi baada ya kufanyika kwa mashambulizi nya mpakani.

Jinsi mashambulizi yalivyoanza

Iran ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya watu wanaoshukiwa kuwa ni waasi katika ardhi ya Pakistan mwezi Januari. Tehran baadaye ikasema kuwa ililenga kundi la wanamgambo wa Kisunni la Jaish al-Adl, ambalo linatajwa kuhusika na mashambulizi kadhaa dhidi ya raia na wanajeshi nchini Iran.
Baada ya hapo Pakistan ililipiza kisasi kwa shambulio dhidi ya kijiji cha Irani karibu na mji wa Saravan, Na yenyewe ikisema kuwa ilikuwa ikilenga wapiganaji wa kundi lililojitenga la Balochistan Liberation Front(BLF).

Jaish al-Adl na BLF ni makundi ya wanamgambo wanaotaka kujitenga na yanayopigania uhuru wa Balochistan, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini linalozunguka mpaka wa Iran na Pakistan. Ingawa kundin la BLF lenyewe halina halina mielekeo ya kidini.

Mkoa wa Balochistan wa Pakistani ndio sehemu kubwa zaidi ya eneo hilo, ukifuatwa na majimbo ya Sistan na Balochistan kwa upande wa Iran. Eneo hili lina wakazi wachache wapatao milioni 9, ambao wanaishi kwa makabila.

 Pakistan
Rais wa Iran akikagua garide katika ziara yake nchini PakistanPicha: EPA/Prime Minister Office

Soma zaidi. Takriban watu 34 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya Marekani nchini Iraq na Syria

Juhudi za uhuru au uhuru katika eneo hilo zimekuwa zikikandamizwa kwa nguvu kutoka kwa pande zote mbili kwa miongo kadhaa sasa. Katika miaka ya hivi karibuni, wabaloch wamezidi kupaza sauti zao huku wakizishutumu serikali za pande mbili kwa ubaguzi na kwa kupora eneo lao.

Kufuatia mashambulio hayo ya mpakani, Iran na Pakistan zilikubali kupunguza hali ya wasiwasi na kuimarisha uhusiano wa kiusalama.
Kama sehemu ya maelewano hayo, walikubaliana kupambana na ugaidi ndani ya maeneo yao na kuanzisha mfumo wa mashauriano katika ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje ili kusimamia maendeleo katika sekta mbalimbali.

Ziara ya Raisi ni ya  kimkakati

Ahsan Raza, mchambuzi wa masuala ya kisiasa mwenye makao yake mjini Lahore, anaamini kuwa safari ya Raisi ina maana ya kurekebisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili. 

Ziara ya Raisi inakuja wakati ambapo nchi hiyo ikiwa kwenye mvutano baada ya Iran kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel. Hatua ambayo Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ameiunga mkono.

"Wewe na nchi yako mmechukua msimamo mkali sana juu ya Gaza, dhididi ya ukatili na unyanyasaji wa kinyama ambao wanafanyiwa Watu wa Gaza. Pakistan pia inasimama pamoja na kaka na dada zetu wa Kipalestina huko Gaza''. amesema Shehbaz.

Ingawa ziara hiyo ilipangwa hata kabla ya mzozo wa Iran na Israel, wachambuzi wa kisiasa wanaamini kuwab Tehran inatafuta uuungwaji mkono wa kimaadili na kidiplomasia wa Islamabad huku kukiwa na hofu ya kuzuka kwa mizozo ya kikanda.

Soma zaidi. EU ministers to discuss air defence for Ukraine, Iran sanctions 

Iran ina uhusiano mzuri na China, Urusi na baadhi ya mataifa ya Asia ya Kati, Akram alidokeza, akibainisha kuwa Tehran pia inataka Pakistan ijiunge na orodha hii ya mataifa rafiki.

Ebrahim Raisi
Rais wa Iran Ebrahim RaisiPicha: Vahid Salemi/AP/dpa/picture alliance

Talat A. Wizarat, mtaalam wa mahusiano ya kimataifa huko Karachi ameiambia DW kuwa Iran inataka Pakistan iiunge mkono Tehran kisiasa na kidiplomasia na kama hilo halitowezekana basi Pakistan iepuke kuwa sehemu ya hatua au mpango wowote dhidi ya Iran.

Moja ya miradi ya pamoja ya hali ya juu ya nchi hizo ni mkataba uliokwama wa usambazaji wa gesi, uliotiwa saini mwaka 2010, ambapo nchi hizo jirani zilikubali kujenga bomba kutoka eneo la gesi la Iran la Fars Kusini hadi mikoa ya kusini mwa Pakistan ya Balochistan na Sindh.

Licha ya Pakistan kuhitaji gesi, Islamabad bado haijaanza ujenzi wa sehemu yake ya bomba hilo, kutokana na hofu ya vikwazo vya Marekani. Iran sasa inaitishia Pakistan kwa hatua za kisheria ikiwa itashindwa kujenga sehemu ya Pakistani ya bomba hilo ingawa Islamabad tayari ilikuwa imetoa idhini ya ujenzi wa kipande cha bomba cha kilomita 80.

Na baada ya kutoa idhini hiyo Marekani imesema haiungi mkono mradi huo na kwamba inaweza kuiwekea vikwazo nchi hiyo ambayo inakabiliwa na madeni .