Moja kwa moja kutoka nyumbani kwa mabingwa wa soka wa dunia, Ligi ya Ujerumani, Bundesliga, inakujia sasa nyumbani kwako barani Afrika kupitia radio Deutsche Welle na washirika wake.
Kila Jumamosi Idhaa ya Kiswahili ya DW inakuletea pambano la kukata na shoka la ligi ya Ujerumani Bundesliga ambapo tunakuchagulia pambano ambalo linavutia kwa vigezo maalumu.
Jumamosi hii (21.04.2018) tumekuchagulia mechi kati ya RB Leipzig dhidi ya TSG Hoffenheim itakayochezwa katika uwanja wa Red Bull Arena mjini Leipzig.
Wenyeji RB Leipzig wako katika nafasi ya 5 na pointi 47 wakati Hoffenheim ikiwa katika nafasi ya 6 na pointi 46 zote zikiwania kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.
Kwa hisia na vitendo kutoka kwa baadhi ya wachezaji bora duniani, Bundesliga itakuwa na kila kitu cha kukufurahisha ikiwa ni pamoja na taarifa muhimu za wachezaji. Nchi wanazotoka, wamecheza mara ngapi katika Bundesliga na kadhalika.
Katika Deutsche Welle Bundesliga Live, unaweza sasa kusikiliza mapambano hayo kwa Kiswahili. Jiunge nasi kila Jumamosi saa 11.25 jioni kwa saa za Afrika mashariki, ili kupata matangazo hayo ya Bundesliga Live.
Kutana na watangazaji wako Sekione Kitojo, Josephat Charo, Bruce Amani, Jacob Safari na Isaac Gamba wakiwa na mchambuzi aliyebobea katika Bundesliga, Ramadhan Ali.
Washirika wetu
Unaweza kusikiliza matangazo haya kupitia redio washirika wetu Afrika mashariki na kati.
Nchini Tanzania kupitia:
Dar es Salaam: Capital FM, Mlimani FM, Wapo Radio
Mkoani Kagera: Fadeco Community Radio na Kasibante FM Radio
Tanga: Mwambao FM
Mwanza: Radio Free Africa na Radio SAUT FM STEREO na Kiss Fm
Mtwara: Pride FM na Safari FM
Mbeya: Ushindi Radio
Arusha: Triple A FM
Moshi: Radio Sauti ya Injili
Mpanda: Mpanda FM Radio
Kahama: Kahama FM
Iringa: Overcomers FM
Kenya washirika wetu ni:
Nairobi: Radio Maisha
Webuye: Radio Mambo
Lamu: Sifa FM
Kapenguria: North Rift Radio
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo:
Uvira: Radio Ondese
Bunia:RTM
Lubumbashi: Radio Phoenix
Uganda washirika wetu ni:
Tororo: Veros Radio
Mbale: Signal FM
Na kupitia satalaiti: SES-5 na Eutelsat 5W
Matangazo ya moja kwa moja katika mtandao wa intaneti unaweza kuyasikia ukibonyeza link chini. Ni wakati matangazo yakiwa yanaendelea tu.