1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dushanbe.Upigaji kura kumchagua rais wafanyika nchini Tajikistan.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvb

Wapiga kura wa nchini Tajikistan leo hii watateremka vituoni kumchagua Rais mpya wa nchi hiyo.

Rais wa sasa wa nchi hiyo, Imomali Rakhmonov anatarajiwa kushinda uchaguzi huo katika kipindi chake cha saba.

Akiwa katika madaraka tangu mwaka 1992, Rais Rakhmonov amekuwa akilalamikiwa na wapinzani na waangalizi kutoka nchi za Magharibi kwa kushindwa kuitishwa uchaguzi huru katika jimbo hilo la zamani la Kisovieti.