Duru ya II ya kombe la Afrika | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 01.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Duru ya II ya kombe la Afrika

duru ya pili ya kombe la Afrika inaanza jumapili hii kwa Ghana ikiwa na miadi na Nigeria na ivory Coast na Guinea.

Tunisia mabingwa wa Afrika 2004 na Angola itakayoandaa kombe lijalo la Afrika 2010 zimenyakua jana tiketi 2 za mwisho za duru ijayo ya kombe la Afrika la Mataifa baada ya kuachana sulubhu 0:0.

Kwa matokeo hayo, Bafana Bafana-Afrika Kusini na Senegal,zinafunga virago kurejea nyumbani mikono mitupu.

Leo nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba anakabiliwa na changamoto kali kutoka stadi wa Ghana, Michael Essien na wa Mali, Frederic Kanoutekatika kinyan’ganyiro cha nani leo mjini Lome, Togo atavaa taji la „mwanasoka bora kabisa wa mwaka wa Afrika.“

Tunisia na Angola zilizotoka jana sare 0:0 mjini Tamale, na kwa tofauti ya magoli-Tunisia imeparamia kileleni mwa kumndi D.

Kwahivyo, mabingwa hao wa 2004-tunisia wana miadi jumatatu ijayo na simba wa nyika-Kamerun.

Duru ya kutoana ya robo-finali itaanza lakini jumapili hii kwa wenyeji Black Stars Ghana kutoana jasho tena na mahasimu wao wa jadi- Super Eagles-Nigeria. Hatima ya kocha wa Ghana-mfaransa Claude Leroy itategemea mpambano huo sawa na ile ya Berti Vogts-kocha wa Nigeria na zamani wa Ujerumani.Ikitimuliwa Ghana na mapema nje ya kombe la Afrika na mahasimu wao Nigeria, sijui mji wa Accra utakuaje baada ya firimbi ya mwisho jumapili hii .

Angola, pia ina kibarua kizito jumatatu hii: Ikiwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Africa Cup, Angola imeingia robo-finali na kutamba mbele ya mabingwa 2 wa zamani wa Afrika-Afrika Kusini na Tunesia, inakumbana na mabingwa watetezi-Misri. Kocha wa Angola Luis Oliveira amedai jana kwamba ,jinsi angola ilivyocheza katika kombe hili la Afrika ,timu yake imeweka Angola katika ramani ya dimba .

Mjini Kumasi jana, Bafana Bafana iliaga kombe hili la 26 la Afrika baada ya kutoka sare bao 1:1 na simba wa Terange-Senegal.Kwa matokeo hayo, wenyeji wa kombe lijalo la dunia-Afrika kusini wamemaliza mkiani kabisa mwa kundi lao.

Nahodha wa Ivory Coast yenye miadi jumapili hii na Guinea-Didier Drogba ,ananyan’ganyia leo mjini Lome taji lake la pili la „mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika“.Drogba lakini anabidi kuzima changamoto ya stadi mwenzake wa Chelsea,Michael essien wa Ghana ,lakini pia Frederic Kanoute wa Mali, anatazamia kuwa leo ni zamu yake kuvaa taji l hilo mjini Lome.

 • Tarehe 01.02.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D0ob
 • Tarehe 01.02.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/D0ob

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com