Duisburg yaingia fainali ya kombe la Ujerumani
2 Machi 2011Duisburg sasa inasuburi mshindi kati ya Bayern Munich na Schalke 04 zinazopambana hii leo katika nusufainali nyingine ya michuano hiyo.
Mabao ya Duisburg iliyokuwa nyumbani yaliwekwa wavuni na Stefan Maierhofer na Srdjan Baljak, huku lile la Cottbus likifungwa na Nils Petersen.
Kuweza kuingia nusufainali Duisburg iliziondoa timu za daraja la kwanza FC Cologne na Kaiserslautern.
Kocha wa Duisburg Milan Sasic ambaye aliingia Ujerumani mwaka 1991 akikimbia vita, na kufanyakazi za kawaida kwa muda wa miaka mitatu, alisema kuwa ushindi huo ni kama ndoto iliyokuwa kweli.
´´Baada ya kazi ya kuijenga timu, sikuwahi kufikiria, kitu kama hiki kinaweza kutokea, kamwe sitoweza kusahau wapi mwanzoni nilipokuwa.Tumemudu kuifanya ndoto yetu kuwa kweli na kupiga hatua kubwa´´alisema kwa furaha
Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA
Mhariri:Mohamed Abdulrahman