DUBLIN: Ahern atazamiwa kubakia madarakani Ireland
26 Mei 2007Matangazo
Nchini Ireland,yadhihirika kuwa Waziri Mkuu Bertie Ahern atabakia madarakani kwa awamu ya tatu.Baadhi ya kura zilizohesabiwa zaonyesha kuwa chama chake cha Fianna Fail kimeshinda uchaguzi uliofanywa siku ya Alkhamisi.Matokeo ya mwisho yanatazamiwa kutangazwa baada ya saa chache.