1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

DRC: Idadi ya waliofariki kwa Ebola yaongezeka

Shirika la afya ulimwenguni,WHO limesema idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Kongo imeongezeka mara dufu na kufikia 62 kwa kipindi cha wiki moja iliopita.

Hata hivyo shirika la WHO limesema ugonjwa huo umebaki kwenye eneo moja pekee huko Djera ,jimboni Equateur. Changa moto kubwa hivi sasa ni kampeni ya kuhamasisha wakaazi wa maeneo hayo ambapo baadhi ya wanaougua wanajificha,limelezea shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka,MSF. Kamati ya pamoja ya madaktari wa Kongo,na wale wa mashirika ya kimataifa imezidisha huduma kwa wagonjwa na watu waliowasiliana na wagonjwa hao mnamo kipindi cha wiki tatu iliopita.Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Salehe Mwanamilongo

Mhariri: Saumu Yusuf

Sauti na Vidio Kuhusu Mada