1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund kileleni mwa Ligi baada ya kuifunga Hoffenheim 3-1

30 Septemba 2023

Borussia Dortmund imechupa kileleni mwa Ligi Kuu ya Bundesliga kwa mara ya kwanza tangu mechi ya mzunguko wa mwisho wa msimu uliopita kwa kuitandika Hoffenheim 3-1 licha ya kumaliza mechi hiyo wakiwa na wachezaji 10.

https://p.dw.com/p/4WzUh
Mchezaji wa Dortmund Felix Nmecha akikabwa na Aster Vranckx katika mechi ya Bundesliga
Mchezaji wa Dortmund Felix Nmecha akikabwa na Aster Vranckx katika mechi ya BundesligaPicha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Vijana wa kocha Edin Terzic walichukua uongozi wa mapema kunako dakika ya 18 ya mchezo kupitia bao la kwanza la mshambuliaji wao mpya Nicklas Fullkrug, japo Hoffenheim ilikomboa dakika saba baadaye kupitia mkwaju wa penalti uliotiwa kambani na Andrej Kramaric.

Marco Reus alifunga bao la pili kabla ya beki Julian Ryerson kufunga la tatu kunako dakika tano za majeruhi.

Leo Jumamosi, mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la Ujerumani DfB Pokal RB Leipzig watakuwa wenyeji wa Bayern Munich katika dimba la Red Bull Arena.

Mshindi wa mechi hiyo ataipiku Dortmund yenye alama 14 hadi nafasi ya kwanza.