1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DILI: Zoezi la kupiga kura lakamilika

9 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCB4

Zoezi la uchaguzi limefanyika leo hii nchini Timor Mashariki kumchagua rais mpya atake chukua mahala pa rais Xanana Gusmao ambae anaachia madaraka.

Hii ni mara ya kwanza kufanyika uchaguzi tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka Indonesia mwaka 2002.

Waziri mkuu Jose Ramos Horta ambae pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel anatarajiwa kuibuka mshindi dhidi ya wagombea wengine saba.

Wachunguzi katika uchaguzi huo wamesema kwamba idadi kubwa ya watu walijitokeza kupiga kura hata ingawa wametaja kujitokeza kasoro chache katika uchaguzi huo.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa rasmi tarehe 16 mwezi huu wa April lakini matokeo ya awali huenda yakaanza kutangazwa hapo kesho.