DILI: Rais mpya ameapishwa Timor ya Mashariki
20 Mei 2007Matangazo
Jose Ramos-Horta ameapishwa kama rais wa Timor ya Mashariki baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi uliofanywa takriban majuma mawili yaliyopita. Katika hotuba yake ya kwanza bungeni,ameahidi kulinda amani na umoja wa taifa.Wakati huo huo alitoa wito kwa makundi hasimu yanayofanya ghasia mitaani,yakomeshe fujo hizo.Hii leo mtu mmoja aliuawa katika mapambano ya makundi hayo.Ramos-Horta alieshinda Tuzo ya Amani ya Nobel katika mwaka 1996,alishinda uchaguzi uliofanywa tarehe 9 Mei kwa kujikingia takriban asilimia 70 ya kura zilizopigwa.Uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanywa mwezi Juni utaamua nani atakaeshika wadhifa wa waziri mkuu.