Dick Cheney azuru Baghdad | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Dick Cheney azuru Baghdad

Makamo-rais wa Marekani Dick Cheney,alipitisha usiku wa jana mjini Baghdad akiwa kiongozi wa kwanza kabisa mkuu wa Marekani kuthubutu kufanya hivyo.

Makamo-rais wa Marekani Dick Cheney,akiwa ziarani nchini Iraq, jana aliwahimiza viongozi wa serikali ya Irak kufanya juhudi zaidi kupunguza machafuko na kuleta masikizano ya kisiasa.Ziara yake hatahivyo, iligubikwa na vishindo vya miripuko iliotikisa madirisha hata katika Ubalozi wa Marekani alipokuwapo humo.

Makamo rais wa Marekani Dick cheney, aliungama huko Baghdad jana kuwa Irak imo kwenye mashaka makubwa ya hali ya usalama lakini alisema kuwa viongozi wa Irak wanaamini hatahivyo, wanafanya maendeleo.lakini pia wana njia ndefu ya kwenda.

Cheney alilitaka Bunge la Irak liache mpango wake wa kwenda likizoni kwa miezi 2 kwa majira ya kiangazi wakati ambapo majeshi ya Marekani yanapigana nchini.

Maswali mengi yakihitaji kupatiwa majibu pamoja na jinsi gain kugawana utajiri wa mafuta ,kuchelewesha mambo zaidi hakuelezeki-alisema Cheney.

Huku nyumbani Marekani wajumbe wa chama cha Upinzani cha democrat wakichachama kudai vita hivi vya miaka 4 sasa vikomeshwe na wanajeshi wa Marekani wafunge virago vyao kurudi nyumbani na umaarufu wa rais george Bush ukizidi kupungua katika uchunguzi wa maoni,Ikulu yake inajikuta sasa inazidi kutiwa shindo ili kuonesha kweli, serikali ya waziri mkuu Al maliki inafanya maendeleo katika hatua zake za kurejesha suluhu nchini na kutekeleza hatua zilizoekewa kuzitimiza na Washington.

Cheney, jana amekuwa kiongozi wa kwanza wa hadhi ya juu kabisa wa Marekani kuthubutu kupitisha usiku mzima nchini Irak tangu Marekani kuongoza uvamizi kuupindua utawala wa marehemu Saddam Hussein,hapo Machi 2003.

Cheney alilala katika kambi ya wanajeshi wa kimarekani kaskazini mwa Baghdad. Cheney alipitisha usiku katika kambi ya camp Speicher,maili 7 kutoka Tikrit, mji alikotoka marehemu Saddam Hussein.Kambi hii imechukua uwanja wa chuo kikuu cha wanahewa wa Irak na ndio kambi ya kiasi cha wanajeshi 10.000 hadi 12.000 wa kimarekani.

Shambulio la mwisho kali katika kambi hiyo lililengwa miaka 2 nyuma na mhanga pekee alikuwa

Raia aliepata pigo la moyo kwa mstuko.

Wakati wa ziara ya Dick Cheney, huko Afghanistan katika kambi ya wanajeshi wa Kimarekani wiki chache nyuma,mtu alijiripua si mbali sana na pale alipokuwapom makamo huyo wa rais wa Marekani alipokuwapo.

Kambi hii alikopitisha usiku wa jana Dick cheney, inalindwa vilivyo na meja Tage Rainsford aliopo katika kambi hiyo amenukuliwa kusema,

“Ninamuambia mama yangu,nina usalama zaidi hapa kuliko nyumbani.” Meja Rainsford anatoka New York lakini maskani yake sasa ni Colorado,Marekani.

Dick Cheney, ameanza jana mjini Baghdad,ziara yake ya Mashariki ya kati .

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com