Waswahili wana tabia ya kuhifadhi historia ya matukio mbalimbali kwenye maisha kwenye majina ya watoto wao, lakini kisiwani Pemba wanahifadhi pia kwa kutumia chakula. Mtafiti wa Lugha na Mahusiano ya Kijamii, Nathalie Arnold, kutoka Marekani, anaelezea kile ambacho amekigundua kisiwani Pemba.