1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA:Fujo zazidi kuendelea Bangladesh.130 wajeruhiwa

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCc8

Kiasi cha watu 130 wamejeruhiwa huku 150 wakikamatwa kufuatia fujo zinazoendelea nchini Bangladesh kwa siku ya pili kati ya polisi na wanaharakati.

Polisi wa kutuliza fujo walifyatua mabomu ya kutoa mamchozi na risasi za mpira kwa maelfu ya wandamanaji waliyokuwa na mawe katika mji mkuu wa Dhaka.

Waandamaji hao wamekuwa wakidai kubadilishwa kwa mfumo uchaguzi na pia kutaka kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu nchini humo uliyopangwa kufanyika mwezi huu.