1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Deutsche Bahn yahofia nyongeza ya mshahara italiathiri shirika hilo

16 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CqD9

BERLIN:

Shirika la reli la Ujerumani la Deutsche Bahn limesema kuwa ile nyongeza ya asili mia 11 ya mshahara waliopewa wafanya kazi juzi itaharibu kazi na kupandisha gharama na pia kuathiri uchumi.

Mkurugenzi Tendaji wa shirika hilo-Hartmut Mehdorn - amesema kuwa mapatano yaliyofikiwa na chama cha madereva wa Treni yatasababisha kupanda kwa bei ya nauli na kufungwa kwa vituo kadhaa.Mvutano kati ya chama cha madereva hao wa treni na shirika la reli la Ujerumani, linalomilikiwa na serikali, ulianza mapema mwaka jana na kusababisha migomo nchini kote ambapo madereva wa treni zaidi ya 5,000 walikuwa wakigomea kazi mara kwa mara mwaka jana.