1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

De Maiziere ndiye waziri mpya wa ulinzi

Abdu Said Mtullya2 Machi 2011

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Thomas de Maizere, leo ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi, baada ya kujiuzulu hapo jana kwa waziri wa hapo awali, Karl-Theodor zu Guttenberg, kwa shutuma za kukopia maandishi.

https://p.dw.com/p/10STR
Thomas de Maiziere
Thomas de MaizierePicha: picture-alliance/dpa

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amechukua hatua za haraka kuziba pengo lililoachwa na waziri wake wa ulinzi aliyejiuzulu jana, zu Guttenberg.

Aliekuwa waziri wa mambo ya ndani hadi sasa, Thomas de Maizere, sasa atakuwa waziri wa ulinzi.

Kansela Merkel ameyafanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri baada ya kukiri kwamba alishangazwa na uamuzi wa waziri wake wa ulinzi zu Guttenberg wa kujiuzulu.

Hans-Peter Friedrich
Hans-Peter FriedrichPicha: dapd

Wazizi huyo alifikia uamuzi huo kutokana na kubanwa na baadhi ya wanasiasa, wasomi na vyombo vya habari. zu Guttenberg alipaswa kuondoka kutokana na kukabiliwa na kashfa ya kuchukua kazi za waandishi wengine na kuziingiza katika tasnifu aliyoiandika kwa ajili ya shahada ya uzamivu-PhD katika mambo ya sheria.

Kansela Angela Merkel pia amemteua Hans-Peter Friedrich kuwa waziri mpya wa mambo ya ndani ya Ujerumani. Hadi wakati wa kuteuliwa Hans-Peter Friedrich alikuwa kiongozi wa wabunge wa chama cha CSU.

Mawaziri hao wawili pia wanatoka katika chama cha CSU kilichomo katika serikali ya mseto na chama cha Kansela Merkel CDU na chama cha waliberali FDP.

Chama cha CSU ambacho ni ndugu wa chama cha Kansela Merkel CDU kilikuwa na haki ya kupendekeza jina la waziri mpya wa ulinzi

Angela Merkel
Angela MerkelPicha: AP

Uteuzi wa Thomas de Maizere unahakikisha usawa katika mizani ya mamlaka ndani ya serikali ya mseto.

Mabadiliko yaliyofanyika katikaa baraza la mawaziri pia yatakuwa na mnufaa kwa chama cha CSU kutokana na mageuzi yanayofanyika kwenye jeshi la Ujerumani yatakayosababishwa kufungwa kwa vituo kadhaa vya jeshi. Hasa katika jimbo la Bavaria kambi nyingi za jeshi zitaguswa na mageuzi hayo.

Wizara za ulinzi na ya mambo ya ndani ni muhimu kwa chama chaa CSU.

Kwa mujibu wa taarifa Kansela Merkel mwenyewe alianzisha mjadala juu ya mabadiliko ya baraza la mawaziri .

Shirika la habari la Ujerumani dpa limearifu kuwaa Merkel angependelea kuona mageuzi ya jeshi la Ujerumani yalifanyika chini ya usimamizi wa mtu anayemwamini - waziri de Maizere

Waziri huyo ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa juu ya mambo ya serikali.Kansela Merkel ana imani kubwa kwamba bwana de Maizere atasonga mbele na utekelezaji wa mageuzi kwenye jeshi la Ujerumani

Kati ya miaka ya 2001 na 2005 de Maizere alishika nyadhifa za fedha, sheria na mambo ya ndani kwa vipindi tofauti katika jimbo la Saxony.

Mwandishi: Abdu Mtullya/DPA/ZAR
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman