Dar Es Salama. Mungano watimiza miaka 43. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Dar Es Salama. Mungano watimiza miaka 43.

Tanzania leo inasherehekea mwaka wa 43 tangu kuasisiwa kwa mungano kati ya Tanganyika na Ungula.

Tanganyika ambayo ni upande wa Tanzania bara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba vilifanya mungano rasmi na kuzaliwa Tanzania.

Pamoja na kutimiza miaka 43 katika mungano huo pande zote mbili kila mara zinaeleza kutoridhishwa kwao kutokana na kuongezwa mambo ambayo hapo kabla waasisi wa mungano huo rais wa zamani wa Tanzania marehemu Julius Kambarage Nyerere na rais wa zamani wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume hawakuyajumuisha.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com