1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Damu inazidi kumwagika nchini Irak

Baghdad:

Watu wasiopungua 17 wameuwawa baada ya bomu kuripuliwa katika mji wa Mahmudiya-kusini mwa Baghdad.Msemaji wa hospitali amesema watu wasiopungua 30 wengine wamejeruhiwa.Inahofiwa maiti zaidi pengine zimefunikwa na magofu.Kuna sababu zinazotofautiana kutokana na mripuko huo wa bomu.Katika wakati ambapo polisi inatzungumzia juu ya kombora lililofyetuliwa,meya wa mji huo anasema bomu limeripuliwa toka ndani ya gari.Maaduka kadhaa yameporomoka kutokana na shambulio hilo.Wakati huo huo Iran imemkatalia waziri mkuu wa Irak NURI el MALIKI ruhusa ya kupita ndege za Irak katika anga ya nchi hiyo.Wakiwa njiani kuelekea Japan,marubani wa ndege ya Irak walitakiwa na Iran wageuze njia kwa hoja ratiba ya usafiri haijatolewa kwa wakati.Ndege hiyo ililazimika kupitia Dubai.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com