1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS : Syria yalaani mauaji ya mbunge wa Lebanone

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrX

Syria imelaani mauaji ya mbunge wa Lebanon anayeipinga Syria Walid Eido kutokana na mripuko wa bomu mjini Bairut Lebanone hapo Jumatano na kukanusha kuhusika na mauaji hayo.

Maelfu ya waombolezaji walipiga mayowe dhidi ya Syria wakati wakilibeba jeneza la Eido kuelekea makaburini mjini Beirut. Washirika wa mbunge huyo wanailaumu Syria kwa mauaji ya mbunge huyo ambaya anakuwa mtu wa saba anayeipinga Syria kuuwawa tokea mwezi wa Februari 2005 wakati Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanone Rafik Hariri alipouwawa kwenye mripuko wa bomu wa kujitolea muhanga maisha kwa kutumia gari mjini Beirut.

Wizara ya mambo ya nje mjini Damascus imesema kampeni ya uzushi imetumiwa na baadhi ya Walebanon kuituhumu Syria kufuatia mauaji hayo.