DAKAR:Rais Wade ashinda uchaguzi matokeo ramsi kutangazwa ijumaa | Habari za Ulimwengu | DW | 28.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DAKAR:Rais Wade ashinda uchaguzi matokeo ramsi kutangazwa ijumaa

Rais wa Senegal Abdoulaye Wade ameshinda uchaguzi war ais uliofanyika mwishoni mwa juma.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na shirika rasmi la habari la APS rais Wade amepata asilimia 55.7 ya kura zilizohesabiwa katika wilaya zote 35 za nchi hiyo ya Afrika magharibi.

Chama kikuu cha Kisocialisti ambacho kimeitawala Senegal kwa miongo mine kabla ya kubwagwa na Wade katika uchaguzi wa mwaka 2000 kinapinga matokeo ya uchaguzi huu.

Hata hivyo matokeo hayo yanabidi kuthibitishwa na tume ya uchaguzi nchini humo kabla ya kutangazwa rasmi siku ya Ijumaa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com