DAKAR:Rais Wade aongoza katika matokeo ya mwanzo ya uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 26.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DAKAR:Rais Wade aongoza katika matokeo ya mwanzo ya uchaguzi

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa Senegal yaliyotangazwa na kituo cha habari cha taifa hii leo yanaonyesha kwamba rais Abdulaye Wade anaongoza kinyang’anyiro hicho dhidi ya wagombea wengine 14 waliojitokeza kupigania kiti cha rais.

Kwa mujibu wa meneja wa Kampeini ya rais Wade pamoja na waziri mkuu wa nchi hiyo,rais Wade amepata asilimia 57 ya kura.

Wasenegal walijitokeza kwa wingi kupiga kura hapo jana jumapili ambapo rais Wade alisema ana imani ya kupata asilimia 50 ya kura ambayo itamuwezesha kutabakia madarakani kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Kiasi waangalizi 2000 wakiwemo 500 wakimataifa walisimamia uchaguzi huo wa Senegal taifa mojawapo la Afrika lililotulia katika demokrasia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com