1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR: Rais wa Senegal anagombea awamu ya pili

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOZ

Uchaguzi wa rais unafanywa hii leo nchini Senegal.Katika baadhi ya maeneo,tangu asubuhi mapema watu walijipanga mistarini hata kabla ya kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura.Rais Abdoulaye Wade anaepigania kubakia madarakani kwa awamu ya pili,anakumbana na wagombea wengine 14. Inasemekana kuwa changamoto kali inatoka kwa waziri mkuu wa zamani,Idrissa Seck ambae huungwa mkono na wapiga kura vijana.Wapinzani wa Wade wanasema,tangu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 kushika madaraka mwaka 2000,hakufanya vya kutosha kuhusu ukosefu wa ajira ya vijana. Nchi ya Senegal hutazamwa kama mfano mzuri wa demokrasia barani Afrika,kwa sababu ya mfumo wake unaoruhusu vyama vingi vya kisiasa na uhuru wa vyombo vya habari.