DAKAR: Nusu ya vifo vya watoto vinavyoweza kuzuiliwa hutokea Afrika
11 Novemba 2006Matangazo
Nusu ya vifo vya watoto duniani,vinavyosababishwa na maradhi yanayoweza kuzuiliwa, hutokea barani Afrika.Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNICEF- shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto duniani,Bibi Ann Veneman,kote duniani, zaidi ya watoto milioni 10 hufariki kutokana na magonjwa ambayo kwa sehemu kubwa yangeweza kuzuiliwa.Kama watoto milioni 5 hufariki katika nchi za Kiafrika.