1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DÜSSELDORF: Airbus A-380 yaanza ziara ya majaribio

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtK

Ndege ya abiria iliyo kubwa kabisa duniani-Airbus A380 imetua katika mji wa Ujerumani,Düsseldorf kabla ya kuanza safari yake ya jaribio katika nchi mbali mbali duniani.Singapore ni kituo cha kwanza cha ndege hiyo itakayotua katika nchi saba za Asia.Vituo vingine wakati wa safari hiyo ya siku 17 ni Australia,Afrika ya Kusini na Kanada. Hiyo ni hatua ya mwisho,kabla ya ndege hiyo kuweza kupata cheti cha idhini ya kutumika kibiashara.Kwa sababu ya matatizo ya kifundi, shirika la Airbus limelazimika kubadilisha mara tatu ratiba ya kuwasilisha ndege za A380.Sasa ndege hizo zitachelewa kwa hadi miaka miwili.