CUF yamfukuza Hamad Rashid na wenzake
4 Januari 2012Matangazo
Wanachama hao wakiongozwa na Rashid wametiwa hatiani na Baraza hilo kwa kuendesha njama za kukivuruga chama hicho. Othman Miraji amezungumza kwa njia ya simu na mwakilishi wa mji mkongwe wa Zanzibar ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF kwa upande wa Zanzibar, Ismail Jussa, kuhusiana na yaliyojiri kwenye kikao hicho.
Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Saumu Mwasimba