Cote D′Ivoire | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Cote D'Ivoire

Laurent Gbagbo akabiliwa na vikwazo vya kiuchumi.

default

Vurugu zinazidi nchini Cote D'Ivoire.

Jumuiya ya Kimataifa  inatayarisha mpango wa kumwekea vikwazo vya kiuchumi Laurent Gbagbo ili kumshinikiza kuondoka madarakani nchini Cote D'Ivoire. Maafisa na wataalamu wanasema kwamba mpango huo umelenga akaunti kuu za benki. Aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Alassane Outtara, anatambuliwa na wengi kuwa mshindi wa uchaguzi wa awamu ya pili wa urais uliofanyika mwezi uliopoita, lakini rais aliyewahi kuingia madarakani kupitia mapinduzi, Gbagbo, amekataa kuondoka madarakani huku vurugu zikizidi kuongezeka.

NO FLASH Elfenbeinküste Wahl Opposition Protest

Wafuasi wa kingozi wa upinzani Alassane Ouattara wakiandamana mjini Abidjan.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Michele Alliot Marie, amesema ni muhimu kuendeleza shinikizo  hata kama ni kupitia kumuidhinisha Outtara kuwa mtia saini rasmi katika mabenki kwa niaba ya fedha za Cote D'Ivoire.

Kombibild Gbagbo und Alassane Ouattara

Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara.

Ufaransa ambayo iliitawala nchi hiyo, imemuomba Gbabgo kujiuzulu kufikia mwishoni mwa wiki. Umoja wa Ulaya inatayarisha vikwazo dhidi ya wafuasi 18 wa Gbagbo, ikiwemo kuzuwiya akaunti zao za benki na kuwapiga marufuku kupewa visa.

Mwandishi Maryam Abdalla/Afpe

Mhariri:Dahman Mohammed

 • Tarehe 18.12.2010
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/QfFo
 • Tarehe 18.12.2010
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/QfFo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com