Cote d′Ivoire. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 02.01.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Cote d'Ivoire.

Ban Ki Moon akariri kumuunga mkono Alassane Ouattara.

default

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon kwa mara nyingine tena amesema kuwa anamuunga  mkono  Alassane Outtara kiongozi wa Cote d'Ivoire anaetambulika kimataifa.

Rais Laurent Gbagbo mpaka sasa amekataa kuyakubali matokeo ya uchgauzi wa hivi karibuni na kuondoka madarakani. Mzozo huo umezusha ghasia katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Laurent Gbagbo / Elfenbeinküste / Abidjan

Kiongozi wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo.

Katika mazungumzo ya simu, Ban alimueleza Outtara kwamba vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vimeamrishwa kufanya kila kiwezekanacho ili kuweza kuingia maeneo ambako inatuhumiwa kuwa maiti nyingi zimezikwa pamoja.

Kambi ya Outtara imewalaumu wafuasi wa Gbagbo kwa mauaji ya wafuasi wake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com