Copa Amerika:Argentina yailaza Colombia 4-2. | Michezo | DW | 03.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Copa Amerika:Argentina yailaza Colombia 4-2.

Copa Amerika inaendelea huko Venezuela huku Argentina wakijiunga na Mexico katika robo-finali.

Mvua yaendelea kufuja mashindano ya Tennis huko wimbledon,Uingereza, Copa America lakini, laendelea kupambamoto huku jana Argentina iliizaba Colombia mabao 4-2 na Paraguay kuitimua nje Marekani kwa mabao 3-1.Michael Ballack,nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani, amefanyiwa leo opreshini nyengine gotini na dibaji imetoka ya changamoto za kombe la dunia la chipukizi ambamo Afrika yawakilishwa na Nigeria,Zambia,Gambia na Kongo.

Kombe la dunia la vijana likiendelea bado duru ya kwanza, ijumaa hii Julai 6,Kongo ina miadi na Chile kabla haikurudi tena uwanjani siku 3 baadae kuumana na Kanada katika changamoto za kundi A.

Zambia majirani zao watakuwa uwanja ni siku moja kabla hapo alhamisi wakioneshana dimba na Spain.Zambia itarudi tena uwanjani siku 2 baadae Julai 7 kucheza na Uruguay.Zambia ina miadi Julai 8 na Ureno.

Julai 5 au alhamisi hii ni zamu ya Gambia kuteremkas uwanjani na mahasimu wao New Zealand.

Nigeria watakamilisha duru hii hapo Julai 8 watakapojaribu kuwachezesha majapani kindumbwe-ndumbwe.

Orodha pia imetoka ya changamoto za kombe la klabu bingwa barani afrika:

Katika kundi A ijumaa hii ijayo, JS Kabylie ya Algeria ina miadi na FAR Rabat ya Morocco wakati siku moja baadae hapo jumamosi Etoile du sahel ya Tunisia watapambana na Al Ittihad ya Libya.

Ama katika zahama za kundi B hapo jumapili,ASEC Abidjan ya Ivory Coast itawakaribishwa mabingwa Al Ahly ya Misri mjini Abidjan.Al Hilal ya Sudan itakuwa nyumbani na wageni wao Esperence ya Tunisia.

Kombe la Marekani-Copa Amerika linasonga mbele na jana ilikua zamu ya Argentina inayopigiwa upatu mno kutoroka na ubingwa mara hii kutamba.Argentina iliin’goa meno Colombia kwa kuichapa mabao 4-2 huko Caracas,Venezuela.

Paraguay nayo ikazima vishindo vya Marekani kwa mabao 3:1.washindi hao wa jana wanajiunga na Mexico iliitoa Brazil kwa mabao 2:0 kwenye duru ya robo-finali.

Nahodha wa Ujerumani anaeichezea Chelsea Michael Ballack, leo amefanyiwa tena opresheni kurekebisha goti lake-Ballack aliumia mwezi uliopita na hakupona bado sawa sawa.

Stadi wa Brazil,Kaka hataiacha mkono Ac Milan,mabingwa wa sasa wa Ulaya ili kujiunga na mabingwa wa Spain,Real Madrid-hii ni kwa muujibu asemavyo makamo-rais wa Milan Adriano Galliani.

Mchezajio wa kiungo wa samba wa nyika-Kamerun, Geremi amekubali kufunga mkataba wa miaka 3 na New Castle ya Uingereza hii leo.Geremi akisubiri hati ya ruhusa ya kufanya kazi anaiachamkono Chelsea.

Mvua inaendelea kufa mashindano ya ubingwa wa Tennis ya Wibledon,Uingereza:

Hatahivyo,kesho asie na mwana aeleke jiwe.Justine Henin wa Ubelgiji atafufua uhasama wake uwanjani na hasimu yake mkubwa Serena Williams wa Marekani katika robo-finali ya Wimbledon.

Na katika medani ya riadha, bingwa wa rekodi ya dunia wa masafa ya mita 100 Asafa Powell wa Jamaica amejitoa katika mbio za ijumaa hii za Golden League mjini Paris kwa kuumia .Powell aliumia mwezi uliopita wakati wa mashindano ya taifa nyumbani Jamaica.Pia atakosa kukimbia mjini Roma hapo Julai 13, lakini anatumai kuwa fit kwa mashindano ya ubingwa wa dunia hapo august 25 huko Osaka,Japan.

 • Tarehe 03.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbo
 • Tarehe 03.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbo