1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CONAKRY: Raia waandamana nchini Guinea wakimtaka Rais Lansana Conte ajiuzulu.

Watu kiasi watatu wameuawa na wengine kadha wakajeruhiwa kwenye makabiliano kati ya maafisa wa usalama na waandamanaji mjini Conakry,Guinea.

Waandamanaji hao wanamtaka rais wa nchi hiyo, Lansana Conte kung`atuka.

Ghasia zimesambaa katika maeneo kadha ya nchi hiyo baada ya mgomo mkubwa uliotishwa kupinga serikali.

Rais huyo mwenye umri wa miaka sabini na miwili amekuwa akikabiliwa na shinikizo aachie madaraka ili kutoa nafasi ya kuundwa serikali ya mpito.

Lansana Conte alitwaa madaraka baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka elfu moja mia tisa na themanini na nne.

Mgomo ulianza mara baada ya rais huyo kusimamisha kesi dhidi ya watu wawili walioshukiwa kwa wizi wa mamilioni ya fedha za serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com