CONAKRY: Mgomo wasimamishwa nchini Guinea baada ya maridhiano kati ya pande husika.. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CONAKRY: Mgomo wasimamishwa nchini Guinea baada ya maridhiano kati ya pande husika..

Vyama vya wafanyikazi nchini Guinea vimesimamisha mgomo uliokuwa ukiendelea baada ya kuafikiana na serikali ya Lansana Conte imteue waziri mkuu na pia ipunguze bei ya mafuta na mchele.

Wakati wa mgomo huo ulioendelea kwa siku kumi na nane, makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama yalisababisha vifo vya watu hamsini na tisa.

Rais Lansana Conte ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka elfu moja mia tisa na themanini na nne, anakabiliwa na upinzani kwa sababu ya ukosefu wa ajira na pia mfumko wa bei.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com