Colombo.Saba wauwawa katika mapigano huko Sri Lanka. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Colombo.Saba wauwawa katika mapigano huko Sri Lanka.

Wanausalama saba wa serikali ya Sri Lanka wameuwawa na kiasi ya wengine kumi wamejeruhiwa, wakati mapigano na waasi wa Kitamil yalipozuka tena katika nchi hiyo.

Idadi kamili ya maafa kwa upande wa waasi hadi hivi sasa bado haijajulikana.

Muungano wa Tamil Eelam unalilaumu jeshi la serikali kwa kuingia na vifaru kwenye eneo lisilomilikiwa na mtu yeyote la upande wa Mashariki wa nchi hiyo.

Serikali ya Sri Lanka imekanusha madai hayo kwa kusema, waasi ndio walioanza kuingia kwenye eneo hilo.

Mwaka huu pekee, zaidi ya raia elfu tatu, wanajeshi na waasi wameuwawa katika mapambano ya kijeshi na kuyafanya makubaliano ya kusitisha matumizi ya silaha ya mwaka 2002 kuingia dosari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com