COLOMBO: Watu takriban 15 wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 03.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO: Watu takriban 15 wauwawa

Waasi wa Tamil Tigers nchini Sri Lanka wametangaza kwamba raia takriban 15, wakiwemo watoto wanne, wameuwawa na wengine kujeruhiwa katika mashambulio ya angani yaliyofanywa na jeshi la serikali.

Msemaji wa waasi hao amenukuliwa akisema kwamba mabomu yalivurumishwa katika kijiji kilicho wilaya ya Mannar kaskazini mwa nchi hiyo.

Hata hivyo, msemaji wa jeshi la angani amewaambia waandishi wa habari kwamba ndege zao zilikishambulia kituo cha waasi wa Sea Tigers, kitengo cha wanamaji cha waasi wa Liberation Tigers of Tamil Eelam.

Alisema shambulio la pili la angani lililenga sehemu zinazotumiwa na waasi hao kuvurumishia makombora katika wilaya ya Batticaloa mashariki mwa Sri Lanka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com