COLOMBO: Watu kiasi ya 100 wauawa katika shambulio la bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO: Watu kiasi ya 100 wauawa katika shambulio la bomu

Kwa uchache watu 99 waliuawa jana katika shambulio la bomu lililovizia msafara wa basi za wafanyakazi wa meli nchini Sri-Lanka. Watu wengine kiasi ya 100 walijeruhiwa.

Shambulio hilo lilitokea karibu na mji wa Habarana kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Serikali imewalaumu waasi wa Tamil Tigers kuhusika na shambulio hilo ambalo ni miongoni mwa mashambulizi yaliyosababisha mauaji ya watu wengi katika kipindi cha miaka 20 ya mzozo kati ya pande hizo mbili.

Machafuko yaliibuka tena tokea mwezi Julai mwaka huu kwa kukiuka mkataba wa kukomesha mapigano wa mwaka wa 2002.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com