1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Watu kadhaa wauwawa katika mapigano

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBv3

Mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Tamil Tigers kaskazini mwa Sri Lanka yamesababisha vifo vya watu kadhaa kabla ya mazungumzo mapya ya kusimamisha mapigano hayajafanyika.

Mazungumzo hayo ya amani yataendeshwa na mjumbe kutoka Japan.

Mjumbe huyo wa Japan Yasushi Akashi anatarajiwa kuzuru maeneo yanayokabiliwa na mzozo nchini Sri Lanka hapo kesho.

Mazungumzo ya amani yalivunjika mwezi Oktoba mwaka jana.

Wakati huo huo wafanyakazi wawili wa shirika la msalaba mwekundu waliotekwa nyara siku ya ijumaa kutoka kwenye kituo cha gari la moshi mjini Colombo wamepatikana wameuwawa kwa kupigwa risasi.

Maiti zao zimepatika katika mji wa Ratnapura kilomita 100 kusini mwa mji mkuu wa Colombo.

Wafanyakzi hao wa shirika la msalaba mwekundu walitekwa nyara na watu waliodai kuwa ni polisi.