COLOMBO: Wasaidizi wa miradi ya Tsunami wameuawa
3 Juni 2007Matangazo
Wafanyakazi 2 wa Shirika la Msalaba Mwekundu wameuawa baada ya kutekwa nyara nchini Sri Lanka. Kwa mujibu wa Msalaba Mwekundu,washambulizi walivaa sare ya polisi.Wafanyakazi hao 2 walikuwa wakishughulikia miradi ya kuwasaidia wahanga wa Tsunami.