COLOMBO: Umwagaji damu waendelea kiswani Sri Lanka | Habari za Ulimwengu | DW | 07.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO: Umwagaji damu waendelea kiswani Sri Lanka

Watu 25 wameuawa katika mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa Kitamil na majeshi ya serikali mashariki na kaskazini mwa Sri Lanka.Kwa mujibu wa maafisa wa jeshi,wapiganaji wa kundi la Tamil Tigers,walishambulia vituo vingi vya kijeshi. Waasi wa Kitamil,tangu zaidi ya miaka 20, wanapigania taifa huru la Kitamil nchini Sri Lanka.Ingawa pande hizo mbili katika mwaka 2002,zilitia saini makubaliano ya kuweka chini silaha,umwagaji damu unaendelea kisiwani Sri Lanka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com