1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Maandamano dhidi ya serikali ya Sri Lanka

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBew

Nchini Sri Lanka,wafuasi wa chama kikuu cha upinzani wameandamana kwa maelfu katika mji mkuu wa Colombo.Waandamanaji hao wanalalamika kuwa serikali imeshindwa kudhibiti bei za bidhaa na rushwa nchini humo.Chama cha UNP kilitayarisha maandamano hayo kwa kuwaleta kama wafuasi 30,000 kutoka kila pembe ya kisiwa hicho,kuandamana katika mji mkuu.Hatua hiyo ni sehemu ya kampeni ya upinzani kuilazimisha serikali ya Rais Mahinda Rajapaksa,kuitisha uchaguzi kabla ya vile ilivyopangwa kufanywa,katika mwaka 2010.Rajapaksa ametupilia mbali uwezekano wa kuwa na uchaguzi wa mapema.