COLOMBO: Afisa wa Tamil Tigers ameuawa Sri Lanka | Habari za Ulimwengu | DW | 03.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO: Afisa wa Tamil Tigers ameuawa Sri Lanka

Kiongozi wa waasi wa Tamil Tigers wa ngazi ya juu ameuawa katika shambulizi lililofanywa na jeshi la anga nchini Sri Lanka.S.P.Thamilselvan alikuwa mkuu wa tawi la kisiasa la Tamil Tigers na vile vile alijitokeza hadharani kama msemaji wa waasi hao.Thamilselvan alikuwa mpatanishi mkuu wa waasi katika majadiliano ya amani yaliyofanywa pamoja na serikali ya Sri Lanka mwezi wa Oktoba mwaka 2006.

Serikali inasema,kifo cha kiongozi huyo ni pigo kubwa kwa waasi lakini kwa maoni ya wachambuzi sasa itakuwa vigumu zaidi kuwakutanisha wajumbe wa Tamil Tigers na serikali ya Sri Lanka.

Tangu mwaka 1983 hadi watu 70,000 wamepoteza maisha yao katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa zaidi ya miaka 20,waasi wa Tamil Tigers wanapigania kujitenga na Sri Lanka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com