Clinton ziarani Afrika Kusini | Matukio ya Kisiasa | DW | 06.08.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Clinton ziarani Afrika Kusini

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton yuko nchini Afrika Kusini akitokea Malawi. Amekutana na rais wa kwanza wa nchi hiyo baada ya utawala wa kibaguzi, Nelson Mandela katika makaazi yake ya kijijini.

default

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham Clinton

Ziara ya Hillary Clinton nchini Afrika Kusini imeanzia kwa chakula cha mchana na Mandela ikiwa ni hatua ya kuonesha jinsi anavyoendelea kupewa heshima kiongozi huyo wa zamani aliyeongoza mapambano dhidi ya utawala wa Wazungu walio wachache.

Mzee Madiba, kama ulivyo umaarufu wa Mandela, ambaye hali yake ya afya yake imekuwa mbaya kutokana na umri ni mtu ambaye sio tu anawawakilisha mashujaa wa dunia bali pia ni mtu ambaye Clinton anamuangalia kama rafiki wake wa karibu. Kama alivyosema afisa mmoja wa Marekani ni Clinton amejifunza mengi mno kutoka kwa Mzee Madiba.

U.S. Secretary of State Hillary Rodham Clinton, left, meets with Malawi’s President Joyce Banda at the State House in Lilongwe, Malawi, on Sunday, Aug. 5, 2012, in the first visit to Malawi by any U.S. Secretary of State. (Foto:Jacquelyn Martin, Pool/AP/dapd)

Hillary Rodham Clinton akiwa Malawi

Mandela alichaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia uliowahusisha watu wa rangi na matabaka yote nchini humo mwaka 1994 ikiwa ni baada ya kukaa jela kwa miaka 27 kama mfungwa wa kisiasa chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi ''Apatheid''. Wakati huo mumewe Hillary Clinton, Bill Clinton ndiye aliyekuwa rais wa Marekani, tangu wakati huo familia hizo mbili zikaanza urafiki wa karibu.

Bill Clinton alifanya ziara nyumbani kwa Mandela, Qunu, mwezi uliopita katika mkesha wa sherehe za siku ya kuzaliwa kwake miaka 94 iliyopita.Hillary Clinton alikutana na Mandela kiasi miaka mitatu iliyopita nyumbani kwake Johannesberg ambapo alimpongeza kutokana na ushawishi aliokuwa nao katika maisha yake.

Former president of South Africa Nelson Mandela smiles during a meeting with Britain's Prime Minister Gordon Brown, at a hotel in central London Tuesday June 24, 2008. Mandela is in London to attend events celebrating his 90th birthday which is next month. (ddp images/AP Photo/Dylan Martinez/Pool) ** zu unserem Korr **

Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela

Katika ziara yake hii Clinton amesema Mandela amefanya mengi ya mafanikio sio tu kwa ajili yake binafsi lakini kwa Waafrika Kusini na Ulimwengu kwa ujumla.Masuala anayopanga kuzungumza na viongozi wa kisiasa akiwa katika ziara hiyo ni pamoja na ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na Afrika Kusini.

Ziara hiyo itakamilika alhamisi ambapo waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani ataelekea Nigeria na Benin.Aidha anatazamiwa kufika Ghana kuhudhuria maziko ya kitaifa ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Atta Mills kabla ya kwenda Uturuki kwa ajili ya mazungumzo juu ya mgogoro wa Syria.

Mwandishi: Saumu Mwasimba

Mhariri: Mohammed Khelef

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com